.
Sera ya Kucheza Kamali kwa Wajibu
Media Bay Limited (“Kampuni” kama ilivyofasiliwa kwenye Vigezo na Masharti) ina wajibu wa kufanya kila liwezekanalo kuwapatia wateja uchezaji mzuri wa michezo ya kubashiri, huku ikitambua kwamba kamali inaweza kusababisha matatizo watoto. Ili kuhakikisha kwamba unaendelea kufurahia uchezaji salama na tiifu, tunaunga mkono kwa ukamilifu Kucheza michezo kwa wajibu.
Ili kuepusha shaka yoyote, tafadhali tambua kwamba neno “Wewe”, “Mchezaji” na “Mteja” yamerejelewa katika sera ya sasa zina maana sawa ( na yamefasiliwa katika Vigezo na Masharti ambayo kwayo sera ya sasa ni sehemu yake).
 1. Tathmini Binafsi ya Michezo ya Kubashili na Mashirika ya Misaada
  1. Tunahimiza na kuwasaidia wateja wetu kuwa makini katika kutambua tabia ya uchezaji wa michezo ya kubahatisha kulikokithiri na kutafuta msaada wa uraibu wa michezo ya kubashiri na matatizo yanayohusiana na hayo.
  2. Kwa msaada katika kutambua iwe ni kuboresha au kutafuta msaada kwa ajili ya tabia yako ya kucheza michezo ya kubashiri, tunakushauri ukamilishe jaribio la tathmini binafsi ili kutathmini kwa uadilifu zaidi na kuelewa vizuri zaidi viwango vyako vya sasa vya uchezaji.
  3. Iwapo wewe au mtu mwingine unayemfahamu ana tatizo la uchezaji wa michezo ya kubashiri tunakushauri kupata msaada kutoka kwa mashirika yanayotambuliwa yaliyotajwa hapo chini:
   • Gamcare – Jaribio la Tathmini Binafsi
Tovutii: https://www.gamcare.org
 • Gamblers Anonymous - Usaidizi na Msaada wa Uraibu wa Michezo ya Kubashiri
Tovuti: http://www.gamblersanonymous.org
 • GambleAware – Jinsi ya Kucheza Micheza ya Kubashiri kwa Wajibu
 
 1. Dhibiti Matumizi yako
Tunawahimizi wateja wetu wote kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa akaunti wa michezo ya kubashiri na hivyo kuwapatia vipengele mbalimbali vya kucheza michezo ya kubashiri kwa wajibu.
 1. Mipangilio ya Ukomo wa Amana na Ukomo wa Madau
 
Fanya udhibiti wa kifedha wa akaunti yako ya michezo ya kubashiri ukiwa na uwezo wa kuweka ukomo uupendao wa kuweka amana na ukomo wa madau. Ukomo wa Amana na Ukomo wa Dau unaweza kuwekwa kwa kipindi kifuatacho:
 • Kwa siku
 • Kwa Wiki (Jumatatu hadi Jumapili)
 • Kwa Mwezi (mwezi wa kalenda)
Unapoomba, ukomo wa amana unaweza kupunguzwa, kuongezwa au kuondolewa kabisa. Kuongezeka au kuondolewa kabisa kwa ukomo wa amana kutaanza kufanya kazi baada ya angalau kipindi cha saa 24 za mapumziko, huku kupungua kwa ukomo wa amana kunaweza kuanza kufanya kazi papo hapo.
Iwapo ungependa kuweka au kurekebisha ukomo wa amana, tafadhali wasiliana na Huduma kwa Wateja / su[email protected] kwa msaada.
Njia za ukomo wa kuweka pesa zitapatikana kwa miamala ya mtandaoni pekee. Iwapo unahitaji usaidizi wa kusimamia shughuli zako unapoweka pesa kwa njia nyinginezo ambazo si za mtandaoni, tafadhali tumia njia za ukomo wa kuweka dau au kupoteza.
 
 1. Ukomo wa Hasara
 
Fanya udhibiti wa kifedha wa akaunti yako ya michezo ya kubashiri ukiwa na uwezo wa kuweka ukomo uupendao wa hasara. Ukomo wa Hasara unaweza kuwekwa kwa vipindi vifuatavyo:
 
 • Kwa siku
 • Kwa Wiki
 • Kwa Mwezi (mwezi wa kalenda)
 • Ukomo wa Hasara kwa Mwaka (mwezi wa kalenda)
 
Unapoomba, ukomo wa hasara unaweza kupungua, kuongezeka au kuondolewa kabisa. Upunguzaji au uondoaji kabisa wa ukomo wa hasara utaanza kufanya kazi baada ya kipindi cha saa 48 cha mapumziko, huku kuongezeka kwa ukomo wa hasara kutaanza kufanya kazi papo hapo.
Iwapo ungependa kuweka au kurekebisha ukomo wa amana, tafadhali wasiliana na Huduma kwa Wateja / [email protected] kwa msaada.
 
 1. Vipimo vya Kikao
 
Kwenye bidhaa zetu za michezo ya kubashiri, utendaji wa kipima kikao unakupatia kumbusho ya kiungwana kuhusu muda ulioutumia kicheza. Kumbusho litatokea kwenye skrini kwa dakika 60 (au baada ya muda mfupi kama umeuchagua) baada ya kuweka ubashiri wako wa kwanza, na litakupatia chaguo la kuendelea kucheza au kuondoa programu ya michezo ya kubashiri.
 
 1. Mapumziko (kipindi cha mapumziko)
Tunafahamu kwamba hali binafsi/ya kifedha ya Mteja inaweza kubadilika na kwamba nyakati nyingine inaleta maana kupumzika kidogo kucheza michezo ya kubashiri na unaweza kufanya hivyo kwa kuomba kipindi cha Mapumziko kwa muda wowote uliowekwa tayari hadi kipindi cha juu cha siku 7, ikiwemo kipindi kifuatacho kilichopendekezwa:
 1. Saa 24
 2. Siku 2
 3. Siku 7 / wiki 1
Vipindi vya Mapumziko vilivyo tajwa hapo juu havina ukomo, lakini vimetolewa kama mfano tu, ambapo lazima utambue kwamba unaweza kuomba kipindi cha Mapumziko cha muda wowote kuanzia saa 24 na hadi muda wa juu kabisa wa siku 7.
Mara baada ya kupokea ombi lako, Kampuni itachukua hatua stahiki kuweka zuwio la muda kwenye akaunti yako ya michezo ya kubashiri iliyofunguliwa kwenye Tovuti, hadi pale kipindi cha mapumziko kitakapokwisha.
KUMBUKA: Mara baada ya kipindi cha Mapumziko kwisha, akaunti yako ya michezo ya kubashiri itaamilishwa kiotomatiki. Vinginevo, na unapoomba tu, tutapitia akaunti yako ya michezo ya kubashiri kuangalia uwezekano wa kuamilishwa upya kabla ya kipindi cha mapumziko kuisha na, ikiidhinishwa, ruhusa ya kushiriki itatpkea katika kipindi cha siku ya 7-ya mapumziko.
 1. Acha Kamali – Kuondolewa (Kujiondoa Mwenyewe Kwa Muda au Moja kwa Moja)
Iwapo, katika hatua yoyote, umepata wasiwasi kuhusu tabia yako ya kucheza michezo ya kubashiri, au umefika kiwango ampacho unahisi huweze tena kucheza michezo ya kubashiri kwa usalama, unatakiwa kuacha na tunaweza kukusaidia kwa kukutoa katika ushiriki wa baadae katika Huduma hii (kama ilivyofasiliwa katika Vigezo na Masharti ambayo kwayo sera ya sasa ni sehemu yake) inayotolewa na Kampuni kwenye Tovuti.
Mara baada ya kupokea ombi lako la  Kujiondoa Mwenyewe, tutachukua hatua stahiki:
 1. kukuzuia / kukufungia kushiriki kwenye michezo, kuweka bashiri au kuweka amana kwenye akaunti yako ya michezo ya kubashiri iliyofunguliwa kwenye Tovuti, katika kipindi cha kujiondoa mwenyewe.
 2. kuwasiliana na wewe kuangalia uwezekano wa kukurudishia fedha zozote zilizobakia kwenye akaunti yako, kulingana na masharti yoyote ya madau yaliyosalia na fedha kidogo za bonasi; na
 3. kukuunganisha na shirika lililobobea kwenye michezo ya kubashiri/kituo cha matibau kama ilivyoainishwa katika Sehemu ya 1 ya sera hii;
 4. Kukusajili kwenye Rajisi ya Kujiondoa Mwenyewe.
KUMBUKA: Mara baada ya kujitoa mwenyewe kwa kipindi kilichokusudiwa kwisha, akaunti yako ya michezo ya kubashiri itaamilishwa kiotomatiki. Iwapo ni  kujitoa mwenye kwa muda ambao haujakusudiwa (ambako kutachukuliwa kama kujitoa moja kwa moja) kunapokuwa kumewekwa, akaunti yako ya michezo ya kubashiri itafungwa.
Kampuni itahifadhi rajisi ya wachezaji wote ambao wameomba kujitoa moja kwa moja au kwa muda au kuzuiwa kupata michezo ya bahati kupitia kipindindi cha Mapumziko, ambacho Mwendeshaji atawasilisha, kwenye vyombo vya udhibiti anapoombwa.
Wachezaji ambao wamejisajili katika rajisi iliyotajwa hapo juu wanaweza tu kuomba kuondolewa kwenye rajisi hii baada ya kwisha kipindi cha miezi sita (6) tokea siku wamejisajili katika rajisi husika.
Mara zote wachezaji wanaweza kuomba kubatilisha hatua za kujitoa wenyewe na, hivyo, kutokana na kujiondoa kwao kwenye Sajili ya Kujiondoa Mwenyewe iliyohifadhiwa na Kampuni, ambako kutaanza kufanya kazi mwezi mmoja baada ya kupokea maombi ya wachezaji na iwapo tu wastani wa chini wa kipindi cha miezi sita ya kujitoa mwenyewe kupita (yaani iwapo kipindi cha miezi sita (6) tokea siku ya usajili wao kwenye Rajisi ya Kujitoa Mwenyewe kupita).
Ilimradi masharti yaliyoelezwa katika aya iliyotajwa hapo juu yamefikiwa na maombi ya wachezaji ya ubatilishaji wa hatua za kujitoa mwenyewe na kujiondoa kwao kwenye Rajisi ya Kujitoa Mwenye iliyohifadhiwa na Mwendeshaji kumethibitishwa na Kampuni, madhara ya ubatilishaji huo ni:
 1. Iwapo kujitoa mwenyewe kulikuwa kwa muda fulani uliokusudiwa, akaunti ya michezo ya kubashiri itaamilishwa upya;
 2. Iwapo kujitoa mwenyewe kulikuwa kwa moja kwa moja (yaani kwa kwa muda usiokusudiwa), na kwa sababu akaunti ya michezo ya kubashiri kufungwa, akaunti ya michezo ya kubashiri utafunguliwa upya.
 
Kampuni ina haki ya kufuta ruhusa ya mteja kushiriki kwenye michezo ya kubashiri bila kikomo, iwapo inaamini kwamba mtu huyo ana matatizo ya kucheza kamali.
Iwapo maombi ya wachezaji ya ubatilishaji wa hatua za kujitoa mwenyewe na kujiondoa kwao kwenye Rajisi ya Kujitoa Mwenyewe iliyohifadhiwa na Mwendeshaji hakujaidhinishwa na Kampuni, na kwa sababu hiyo majina yao yataonekana kwenye Rajisi ya Kujitoa Mwenyewe iliyohifadhiwa na Mwendeshaji, iwapo wachezaji watabainika wanajaribu kufungua akaunti mpya za michezo ya kubashiri kwenye Tovuti, Mwendeshaji atazifunga akaunti hizo na jumla ya fedha iliyopo kwenye akaunti za michezo ya kubashiri itanyang'anywa na kuhifadhiwa na Kampuni.
Ikiwa kama hatua ya kuzuia, tunapendekeza kwamba ufikirie kutumia ulinzi uleule wa Kujitoa Mwenyewe kwa waendeshaji wengine wa ambao wanasimamia akaunti zako za michezo ya kubashiri.
Iwapo unahitaji kuacha kucheza michezo ya kubashiri, tafadhali wasiliana na Huduma kwa Wateja / [email protected] kwa msaada wa haraka.
Kampuni haitatuma nyenzo zozote za matangazo ya biashara au masoko kwa wacheza ambao wamejitoa kwa muda au moja kwa moja, au kwa wachezaji ambao wameomba kuzuiwa kushiriki kwenye michezo ya kubashiri kupitia kipindi cha Mapumziko.
 1. Maelezo ya Shughuli
Taarifa inayohusiana na kila vipindi vyako vya mchezo kwenye Tovuti inaweza kuhakikiwa angalau kwa siku 90. Taarifa inajumuisha tarehe ya kuanza na muda wa kipindi chako cha mchezo, pamoja na muda uliotumika. Taarifa zaidi kuhusiana na shughuli uliyokuwa ukiifanya katika akaunti ya michezo ya kubashiri iliyofunguliwa kwenye Tovuti pia inaweza kuhakikiwa kwa kipindi cha angalau siku 90. Taarifa inajumuisha maelezo ya kina kuhusu salio la akaunti yako, historia ya michezo (ikiwemo kiasi cha ubashiri/madau, ushindi na kupoteza),amana, utoaji fedha na miamala mingine kama hiyo.
Aidha, kutakuwa na ujumbe wa onyo utakaotumwa kiotomatiki wakati wa uchezaji mchezo, ukikujulisha kuhusu muda ulioutumia kwenye Tovuti au kwenye mchezo, kila baada ya dakika 60.
 1. Kamali Chini ya Umri
 
Tunachukua hatua kali kuhakikisha kwamba watu wenye umri unaoruhusiwa kisheria tu wanashiriki na kuingia katika tovuti yetu. Uchunguzi huo unajumuisha mchakato wa utambulisho na uthibitisho ili kuthibitisha vyote umri na utambulisho mara baada ya kuingia na kila wakati unapotembelea tovuti yetu. Kwa kila muunganisho wa kwenye tovuti yetu, ujumbe wa onyo kwa watoto unaopinga kujihusisha na kamali utachezwa. Zaidi ya hayo, tunaweza kuwaomba wateja kuwasilisha nakala ya nyaraka za utambulisho zenye picha (hati ya kusafiria au kitambulisho kilichotolewa na serikali), ili kuthibitisha vyote umri na utambulisho.
Maelezo yoyote binafsi tunayokuomba ni ya kuthibitisha utambulisho wako – haya ni matakwa ya kisheria kwa ajili ya ulinzi wako mwenyewe vilevile ulinzi wetu. Iwapo una maswali yoyote kuhusu ukaguzi wetu wa utambulisho, tafadhali usisite kuwasiliana na Huduma kwa Wateja / [email protected] muda wowote.
 
TAFADHALI KUMBUKA KWAMBA YEYOTE MWENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA 18 AKIBAINIKA KUTUMIA TOVUTI HII USHINDI WAKE WOWOTE UTANYANG'ANYWA.
Mifumo ya Uchujaji
 
Mwendeshaji anashauri na kuhimizi wateja wake kuwazuiwa watoto dhidi ya kutumia tovuti za kamali. Huduma ya uchujaji itawasaidia na kuwaongoza wazazi kudhibiti matumizi ya intaneti, kulingana na vigezo husika. Wazazi wanaweza kutumia vichujio kuzuia watoto wao kutumia tovuti za kamali.
 
Iwapo unatumia kompyuta yako na marafiki zako au wanafamili ambao wana umri unaoruhusiwa kisheria kusajili au kubashiri kwenye tovuti zetu, tafadhali fikiria kutumia huduma tarajiwa za uchujaji kama vile:
 
Net Nanny™ www.netnanny.com
 
CyberPatrol www.cyberpatrol.com
 
Mara ya Mwisho Kuboreshwa: [the date when the final version of this policy is agreed upon should be inserted herein]
 
 
Top