Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 Masters Tournament
US PGA Tour
European Tour
Japan Golf Tour
Augusta National Golf Club
Augusta, Georgia, USA
7-10 April 2022
Shindano la gofu la
Masters 2022 linatarajiwa kuchezewa Augusta National Golf Club kati ya tarehe 7 na 10 Aprili.
Haya yatakuwa makala ya 86, na ya kwanza kati ya mashindano manne makubwa kwa upande wa wanaume kuandaliwa mwaka 2022 huku koti la kijani likitolewa kama zawadi kwa bingwa.
Shindano hili lilianzishwa mwaka 1934, ikiwa ni miaka 88 iliyopita. Ni shindano rasmi lililopo kwenye ratiba ya PGA Tour, European Tour na Japan Golf Tour.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Hideki Matsuyama ndiye bingwa mtetezi wa shindano hilo baada ya kuibuka na ushindi mwaka jana kwa jumla ya alama 278 (−10).
Wachezaji wakubwa kama Matsuyama, Jon Rahm, Scottie Scheffler, Collin Morikawa, Rory McIlroy, Justin Thomas, Brooks Koepka na Dustin Johnson watakuwa miongoni mwa washiriki mwaka huu.
Mshindi mara tano wa Masters Tiger Woods atasema baadaye kama atashiriki mashindano ya mwaka huu baada ya kuwa nje ya gofu tangu mwaka 2020.
Washindi wa zamani wa Masters Fred Couples, Patrick Reed, Sergio Garcia, Adam Scott, Charl Schwartzel, Danny Willett, Bernhard Langer, Vijay Singh na Mike Weir pia watashiriki.
Shindano la mwaka 2022 linatazamiwa kuchezwa ndani ya siku nne huku likiwa shindano la 25 katika kalenda ya msimu 2021/22 wa PGA Tour.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Woods hakucheza mwaka 2021 kutokana na ajali ya gari aliyoipata mwaka 2021 na kupata majeraha mabaya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 46 aliandika kwenye mtandao kuwa atasema iwapo atashiriki Masters ya mwaka huu.
“Naelekea Augusta leo kuendelea mazoezi na maandalizi yangu. Nitafanya maamuzi iwapo nitashiriki,” aliandika Woods kwenye mtandao wake wa Twitter Jumapili. Sunday.
Mshindi mara 15 huyo wa mashindano makubwa ya gofu ambaye alishinda Masters mwaka 1997, 2001, 2002, 2005 na 2019 alicheza kujipima nguvu Augusta wiki iliyopita. Jack Nicklaus ndiye mchezaji aliyeshinda Masters zaidi ya Woods huku akiwa ameshinda mara sita.
Washindi watano wa mwisho wa shindano la Masters
2017 - Sergio Garcia - Uhispania
2018 - Patrick Reed - Marekani
2019 - Tiger Woods - Marekani
2020 - Dustin Johnson - Marekani
2021 - Hideki Matsuyama - Japan
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.