16 BORA ULAYA NI ‘UBAYA UBWELA’ MWANZO MWISHO… CITY vs MADRID, ARSENAL MCHEKEA…


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo

DROO ya hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imethibitisha pambano lingine kubwa kati ya Manchester City na Real Madrid katika hatua ya 16 bora. Huu ni mchuano ambao sasa umegeuka kuwa kama “fainali kabla ya fainali” kutokana na historia yao ya hivi karibuni.

Tangu mwaka 2020, timu hizi zimekutana mara kwa mara katika hatua za mtoano. Pambano lijalo litakuwa mara ya sita ndani ya miaka saba kukutana kwenye hatua kubwa za mashindano haya.

Kwa jumla, ndani ya mechi 15 za karibuni, Manchester City wameshinda mara tano, sare nne na kupoteza mara sita dhidi ya Real Madrid. Cha kuvutia zaidi ni kwamba magoli ni sawa kabisa 29 kwa 29, kitu kinachoonesha namna ambavyo wamekuwa wakilingana kwa kiwango.

Mwaka 2020 City waliitoa Madrid katika hatua ya 16 bora kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2. Mwaka 2022 Madrid walirudisha mapigo kwenye nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya 6-5 baada ya muda wa ziada, katika moja ya michezo ya kukumbukwa zaidi katika historia ya Champions League.

Mwaka 2023 City walilipiza kisasi kwa ushindi wa jumla ya 5-1 kwenye nusu fainali kabla ya kwenda kutwaa ubingwa. Mwaka 2024 na 2025 walikutana tena katika robo fainali na hatua ya play-off, mechi ambazo zilijaa mabao na drama ikiwemo mikwaju ya penalti.

Sasa wanakutana tena. Miaka saba, mechi zaidi ya kumi na mbili, idadi ya mabao sawa. Ni rahisi kusema kati yao, hakuna anayemmiliki mwingine hapa,atakayejichanganya ndio huyohuyo.

ARSENAL vs LEVERKUSEN

ARSENAL wamepangwa kukutana na Bayer Leverkusen katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2025/26, droo ambayo tayari imeanza kuvuta hisia kutokana na stori inayomuhusu Kai Havertz.

Havertz, ambaye ni zao la akademi ya Leverkusen, alipandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2016 kabla ya kuhamia Chelsea majira ya kiangazi 2020. Mwaka 2023 akasajiliwa na Arsenal. Sasa anaenda kukutana na klabu iliyomlea kwenye hatua ya mtoano ya Ulaya.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya,Wamekutana mara kwenye mechi 2 tu za msimu wa 2001/02. Leverkusen walitoa sare ya 1-1 nyumbani kabla ya kushinda 4-1 ugenini dhidi ya Arsenal. Msimu huo Arsenal walimaliza wa tatu kwenye kundi lao wakiwa na pointi saba na wakaondolewa, wakati Leverkusen waliongoza kundi kwa pointi 10 na baadaye wakafika hadi fainali ya mashindano ambapo walifungwa 1-2 na Real Madrid.

BARCELONA vs NEWCASTLE

BARCELONA watakutana na Newcastle United katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya droo kufanyika leo kwenye makao makuu ya UEFA mjini Nyon, Uswisi.

Barça walikuwa na uwezekano wa kukutana na timu mbili ambazo ni Newcastle au PSG, na hatimaye wakapangwa dhidi ya klabu hiyo ya Ligi Kuu England. Newcastle wameingia hatua hii wakiwa na morali kubwa baada ya kuiondoa Qarabag kwenye Playoffs kwa ushindi mzito wa jumla ya mabao 9-3.

Timu hizi tayari zilishakutana mapema msimu huu kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya ligi uliopigwa St. James’ Park. Barcelona waliibuka na ushindi wa 2-1, huku Marcus Rashford akifunga mabao hayo.

Kwa kuwa Barcelona walimaliza kwenye nane bora, wamepata faida ya kupiga mechi ya pili nyumbani Camp Nou. Hata hivyo, mtihani mkubwa utakuwa kwenye mchezo wa kwanza England, hasa kwa presha na mazingira ya St. James’ Park.

Changamoto nyingine kwa kocha ni kukosekana kwa Frenkie de Jong, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji bora kwenye mchezo wa kwanza lakini safari hii hatakuwepo kutokana na majeraha.
Nani atamtoa mwenzake mwaka huu?

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 03/02/2026