HATIMAYE, KARIAKOO DERBY KUPIGWA ISAMUYO, VITA YAANZA RASMI


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo


UONGOZI wa Simba SC umetangaza rasmi kuuchagua Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kuwa utakaotumika kwa mchezo mkubwa wa Kariakoo Derby dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, utakaopigwa Mei 3, 2026.

Uamuzi huo ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kujihakikishia mazingira bora ya ushindani, sambamba na kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa mashabiki wanaotarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo lenye historia kubwa nchini.

Simba wanaamini uwanja huo unaweza kuwa kichocheo muhimu cha mafanikio katika mchezo huo huku wakiwa wenyeji wa mechi hiyo.

Wakati maandalizi ya kuelekea derby hiyo yakiendelea, kikosi cha Simba kinaendelea kujifua kwa kasi, huku benchi la ufundi likifanya tathmini ya kina ili kuhakikisha timu inakuwa katika ubora wa hali ya juu ifikapo siku ya mchezo.

Malengo yao makubwa ni kuibuka na ushindi na kuendeleza ubabe mbele ya wapinzani wao wa jadi.
Kwa upande wa Yanga SC, nao wanatarajiwa kuingia uwanjani wakiwa na morali ya hali ya juu, hali inayoongeza uzito wa pambano hilo ambalo kwa kawaida huambatana na ushindani mkali na presha kubwa kwa timu zote mbili.

Kariakoo Derby inaendelea kubaki kuwa moja ya mechi zinazovuta hisia za mashabiki wengi, si tu nchini Tanzania bali pia katika ukanda wa Afrika Mashariki, kutokana na historia yake, ushindani wake na ubora wa vikosi vya timu hizi.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 04/29/2026