Jinsi ya Kucheza Roulette
Roulette ni moja ya michezo ya kasino inayotambulika zaidi duniani, ikiwa na gurudumu linalozunguka, mifuko yenye namba na mpira mdogo. Kabla ya kila mzunguko, unaweka dau kwenye namba, rangi, kundi la namba au matokeo mengine unayodhani yatatokea.
Baada ya muda wa kuweka dau kuisha, gurudumu huzunguka na mpira hutua kwenye moja ya mifuko yenye namba. Mfuko ambao mpira umetua ndiyo huamua matokeo ya ushindi.
Ikiwa unacheza roulette ya kidijitali, matokeo huzalishwa kielektroniki kwa kutumia
Kizalishaji cha Namba za Nasibu -
Random Number Generator (RNG).
Lini ni Lengo la Mchezo wa Roulette?
Lengo la roulette ni kutabiri matokeo ya mzunguko unaofuata.
Kutegemea mchezo unaocheza, unaweza kuweka dau kwenye:
- Namba moja
- Kundi la namba
- Nyekundu au Nyeusi
- Namba Tasa au Shufwa
- Namba za chini (1 hadi 18)
- Namba za juu (19 hadi 36)
- Dazeni (Dozen)
- Safu (Column)
Aina tofauti za dau hufunika idadi tofauti za matokeo yanayowezekana. Dau zinazofunika namba chache kwa kawaida hulipa zawadi kubwa zaidi lakini nafasi yake ya kushinda ni ndogo. Dau zinazofunika namba nyingi kwa kawaida hulipa zawadi ndogo lakini zinaweza kushinda mara nyingi zaidi.
Hakuna dau la roulette linaloweza kuhakikisha ushindi.
Aina za Magurudumu ya Roulette
Aina ya gurudumu la roulette inaweza kuathiri idadi ya matokeo yanayowezekana, hivyo ni muhimu kuangalia sheria za mchezo kabla ya kuweka dau.
Roulette ya Ulaya (European Roulette)
Roulette ya Ulaya ina mifuko 37: namba 1 hadi 36 na sifuri moja (0).
Roulette ya Marekani (American Roulette)
Roulette ya Marekani ina mifuko 38. Mbali na namba 1 hadi 36, ina sifuri moja (0) na sifuri mbili (00).
Sifuri ya ziada hubadilisha uwezekano wa matokeo mbalimbali, ingawa malipo ya kawaida hubaki sawa.
Roulette ya Ufaransa (French Roulette)
Roulette ya Ufaransa kwa kawaida hutumia gurudumu lenye sifuri moja, kama roulette ya Ulaya.
Baadhi ya meza za roulette ya Ufaransa huwa na sheria maalum kama
La Partage au
En Prison, ambazo zinaweza kuathiri dau za malipo sawa (even-money bets) pale mpira unapotua kwenye sifuri. Sheria hizi hutofautiana kulingana na mchezo, hivyo hakikisha unasoma taarifa za meza kabla ya kuweka dau.
Jinsi Raundi ya Roulette Inavyofanya Kazi
1. Chagua mchezo wa roulette
Angalia aina ya gurudumu, viwango vya chini na vya juu vya dau, pamoja na sheria za mchezo kabla ya kuanza.
2. Chagua kiasi cha kucheza
Chagua kiasi unachotaka kucheza kulingana na viwango vya chini na vya juu vinavyoruhusiwa na mchezo. Betway Tanzania huonyesha dau kwa
TSh.
3. Weka dau lako
Chagua namba, rangi, kundi la namba au matokeo mengine yanayopatikana.
4. Muda wa kuweka dau unafungwa
Mara tu muuzaji (dealer) au mchezo unapotangaza kuwa hakuna dau zaidi zinazokubaliwa, hutaweza kuongeza dau kwa mzunguko huo.
5. Gurudumu huzunguka
Mpira huzunguka kwenye gurudumu kabla ya kutua kwenye mmoja wa mifuko yenye namba.
6. Matokeo hutangazwa
Namba na rangi iliyoshinda huoneshwa.
7. Dau zinatatuliwa
Dau zilizoshinda hulipwa kulingana na malipo husika, huku dau zilizopoteza zikitatuliwa kulingana na sheria za mchezo.
Maelezo ya Dau za Ndani - Inside Bets
Inside Bets huwekwa moja kwa moja kwenye sehemu ya namba kwenye meza ya roulette. Hufunika namba chache na kwa kawaida hulipa zaidi.
Aina za kawaida ni:
- Dau la Namba Moja- Straight-up: Hufunika namba moja na kwa kawaida hulipa 35:1.
- Dau la Namba Mbili Zinazopakana - Split: Hufunika namba mbili zinazopakana na kwa kawaida hulipa 17:1.
- Dau la Mstari wa Namba Tatu - Street: Hufunika mstari wa namba tatu na kwa kawaida hulipa 11:1.
- Dau la Kona - Corner: Hufunika namba nne zinazokutana kwenye kona moja na kwa kawaida hulipa 8:1.
- Dau la Mstari wa Namba Sita - Six Line: Hufunika namba sita katika mistari miwili iliyo karibu na kwa kawaida hulipa 5:1.
Uwiano wa malipo unahusu faida ya ushindi pekee. Kiasi cha awali kilichowekwa kwa kawaida hurudishwa tofauti.
Maelezo ya Dau za Nje - Outside Bets
Outside Bets hufunika makundi makubwa ya namba na kwa kawaida hulipa kidogo kuliko Inside Bets.
Aina za kawaida ni:
- Nyekundu au Nyeusi: Hulipa 1:1.
- Tasa au Shufwa: Hulipa 1:1.
- Chini au Juu: Hufunika 1 hadi 18 au 19 hadi 36 na hulipa 1:1.
- Dazeni (Dozen): Hufunika 1 hadi 12, 13 hadi 24 au 25 hadi 36 na hulipa 2:1.
- Safu (Column): Hufunika moja ya safu tatu zenye namba 12 na hulipa 2:1.
Sifuri (0), na sifuri mbili (00) inapohusika, hazijumuishwi katika uchaguzi wa kawaida wa Nyekundu/Nyeusi, Tasa/Shufwa au Chini/Juu.
Jinsi Malipo ya Roulette Yanavyofanya Kazi
Malipo yako yanategemea aina ya dau ulioweka na idadi ya namba inayofunikwa.
Kwa mfano, ukiweka dau la TSh 200 kwenye namba moja na ukashinda kwa uwiano wa 35:1, faida yako itakuwa TSh 7,000. Dau lako la awali la TSh 200 kwa kawaida litarejeshwa pia, na kufanya marejesho yako kuwa TSh 7,200 kwa jumla.
Kumbuka kuwa malipo makubwa kwa kawaida yanawakilisha matokeo yanayotokea mara chache zaidi.
Malipo yanaweza kutofautiana kwa chaguo maalum na dau za ziada. Daima angalia jedwali la malipo lililoonyeshwa kwenye mchezo husika kabla ya kucheza.
Roulette ya Mtandaoni dhidi ya Roulette ya Moja kwa Moja
Unaweza kukutana na matoleo mbalimbali ya roulette kwenye Betway Tanzania Casino.
- Roulette ya RNG: Matokeo huzalishwa kielektroniki kwa kutumia Random Number Generator.
- Roulette ya Moja kwa Moja (Live Roulette): Dealer halisi huzungusha gurudumu la roulette na mchezo huonyeshwa kwa njia ya video ya moja kwa moja.
- Roulette ya Kiotomatiki (Automated Roulette): Gurudumu halisi au la kiotomatiki huunganishwa na mfumo wa kidijitali wa kuweka dau.
Lengo kuu la mchezo hubaki lilelile, ingawa kasi, muonekano, viwango vya dau na aina za chaguo zinaweza kutofautiana kati ya michezo.
Mambo ya Kuangalia Kabla ya Kucheza Roulette
Kabla ya kuweka dau, hakikisha umeangalia:
- Aina ya gurudumu la roulette
- Kiwango cha chini na cha juu cha dau
- Malipo ya dau za kawaida na maalum
- Muda unaoruhusiwa kuweka dau
- Sheria za sifuri (0) na sifuri mbili (00)
- Iwapo sheria maalum za roulette ya Ufaransa zinatumika
- Dau za ziada au chaguo maalum zilizopo
- RTP na sheria za mchezo
Kufahamu sheria za roulette unayocheza kutakusaidia kuelewa jinsi dau lako litakavyoshughulikiwa.
Vidokezo vya Roulette kwa Wanaoanza
Ikiwa wewe ni mchezaji mpya wa roulette:
- Fahamu kila aina ya dau inafunika nini kabla ya kuiweka.
- Angalia kama mchezo unatumia gurudumu lenye sifuri moja au sifuri mbili.
- Weka bajeti kabla ya kuanza kucheza.
- Usidhani kwamba mizunguko iliyopita itaathiri mzunguko unaofuata.
- Kuwa mwangalifu na mifumo inayodai kuhakikisha ushindi.
- Acha kucheza unapofikia muda au kiwango cha matumizi ulichojiwekea.
Kila mzunguko wa roulette ni tukio huru. Mfululizo wa Nyekundu au Nyeusi hautoi uhakika kwamba rangi tofauti itatokea kwenye mzunguko unaofuata.
Cheza Roulette kwa Kuwajibika
Roulette ni mchezo wa bahati nasibu. Kuelewa gurudumu, aina za dau na malipo kunaweza kukusaidia kufuatilia mchezo, lakini hakuwezi kutabiri matokeo yajayo wala kuhakikisha ushindi.
Jiwekee kikomo cha muda na matumizi kabla ya kuanza, usifukuze Hasara na cheza tu kwa pesa unazoweza kumudu kupoteza.
Wachezaji lazima wawe na umri wa miaka 18 au zaidi ili kucheza.
Beti Sasa
TSh MILIONI 10 KUSHINDANIWA. Beti TSh 1,250+, Mechi 3+ Ikijumuisha Mechi ya Simba