Hakimiliki ya picha: Getty Images
Charlotte Hornets v Memphis Grizzlies
2021-22 NBA Regular Season
Sunday 13 February 2022
Spectrum Center, Charlotte, North Carolina
Tip-off at 02:00
The Charlotte Hornets na Memphis Grizzlies watamenyana mnamo Jumapili tarehe 13 Februari 2022 katika mechi ya
NBA, Spectrum Center, Charlotte iliyopo North Carolina. Mechi inatazamiwa kuanza saa nane kamili majira ya Afrika ya kati.
The Hornets wamekwea jedwali la Eastern Confererence polepole na sasa wana matumaini ya kushiriki mechi za mchujo. Tatizo lao moja ni kwamba wamekuwa wakianza mechi vibaya kabla ya kutoka nyuma na kumshinda mpinzani. Hali hii imepelekea kushindwa kwao katika mechi ambazo hawangepoteza.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Tulipambana sana mara nyingi tukiwa katika nafasi za kupoteza mechi,” alisema mchezaji LaMelo Ball. “Kwa sasa upinzani ni mkali. Timu zitapambani hadi mwisho kwa hali na mali ili kucheza mechi za mchujo.” Aliongeza kuwa, “ni sharti wachezaji wetu waongeze juhudi zaidi iwapo tunataka kufika huko.
Kwa upande mwingine, The Grizzlies wamekuwa wakishinda mechi muhimu huko Western Conference na sasa wanawakaribia Phoenix Suns na Golden State Warriors kama timu zitakazoshiriki mechi za mchujo.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Memphis wanajulikana kama timu inayocheza mchezo wao kwa kutumia nguvu sana. "Wapinzani hawana pa kukimbilia,” alisema Ja Morant. “Tutafanya chochote katika hali yoyote kupata ushindi. Hatumuogopi yeyote. Tutawaonyesha uwezo wetu. Tutajituma iwezekanavyo ili kupata ushindi. Haijalishi kama unapenda tunavyocheza mchezo wetu.”
Jaren Jackson aliongeza, “Unafahamu mtindo wetu tunavyocheza. Tunatumia nguvu nana uwepo wetu utasikika uwanjani. Tunapenda kucheza hivyo. Inatuletea raha na kutupa imani kwamba tupo kwenye mashindano makubwa.”
Historia inaonyesha kuwa the Hornets na the Grizzlies wamekutana mara 46 katika NBA tangu 1995-96. Charlotte wameshinda mechi 25 huku Memphis wakishinda mara 21. Mara ya mwisho timu hizi zilikutana Novemba 2021 ambapo the Hornets walishindsa 118-108 wakiwa ugenini. Kelly Oubre Jr alichangia alama 37 katika ushindi huo.
Takwimu baina ya Charlotte Hornets na Memphis Grizzlies, NBA
Mechi: 46
Hornets: 25
Grizzlies: 21
Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.