Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
UONGOZI wa klabu ya Yanga umetuma ujumbe mzito kuelekea mchezo wao wa
Jumamosi, Januari 31 dhidi ya Al Ahly, ameeleza wazi kuwa pambano hilo limebeba hatma ya timu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa kutambua uzito wa mechi hiyo ya maamuzi, kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi maalum ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Al Ahly mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema mechi ya Jumamosi ni karata ya mwisho kwao na haina nafasi ya makosa, akibainisha kuwa ushindi pekee ndio utakaowaweka hai kwenye mbio za kusonga mbele.
“Kuifunga Al Ahly kunahitaji akili, nidhamu na utulivu mkubwa. Tumekuja Zanzibar tukiwa tumepanga kila kitu, hatutacheza na Al Ahly kichwa kichwa kwa sababu waarabu sio watu rahisi kabisa,” amesema Kamwe.
Kamwe ameongeza kuwa Yanga inaufahamu vyema ubora wa Al Ahly pamoja na uzoefu wao mkubwa katika michuano ya Afrika.
Ameweka wazi kuwa benchi la ufundi na wachezaji wake wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanapigania ushindi mbele ya mashabiki wao.
Kwa mujibu wa Kamwe, mchezo wa Jumamosi sio wa kawaida, bali ni vita ya heshima, historia na ndoto ya Yanga kuandika ukurasa mpya katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.