KUELEKEA MECHI NA WAARABU… BEKI ESPERANCE ATAJA MASTAA WA KUCHUNGWA


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo

LICHA ya Simba kupoteza dhidi ya Esperance de Tunis ya Tunisia, lakini Waarabu hao hawawezi kuwasahau nyota watatu wa kikosi hicho cha Msimbazi walioonekana kuwapa wakati mgumu.
 
Simba inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumamosi iliyopita ilikubali kichapo cha bao 1-0 ugenini ikiwa ni kipigo cha tatu mfululizo katika kundi D la michuano hiyo msimu huu. Kabla ya hapo ilifungwa 1-0 na Petro Atletico, kisha ikapigwa 2-1 na Stade Malien.
 
Beki wa zamani wa TP Mazembe, Ibrahim Keita ambaye kwa sasa anakichafua pale Esperance, amesema licha ya kwamba wameifunga Simba, lakini mechi hiyo ilikuwa ngumu dakika zote 90.
 
Amesema kichwani kwa mastaa wa Esperance kuna majina ya wachezaji watatu waliowatesa sana kutokana na viwango vyao bora.
 
“Kuna yule kipa (Djibrilla Kassali), winga aliyeingia namba 29 (Libasse Gueye) na kiungo mkabaji namba 21 (Yusuph Kagoma), viwango vyao uwanjani vilitusumbua wengi.
 
“Nimeifahamu Simba kwa muda, ila uwepo wa mastaa wapya umeongeza mabadiliko makubwa sana ndani ya kikosi hicho.
 
“Unajua mnapocheza na wachezaji wenye viwango vikubwa, basi ni kipimo kizuri cha kutusaidia kujipima kwani mashindano yanaendelea na wapinzani wote wako imara.”
 
Katika hatua nyingine, beki huyo raia wa Mali aliyecheza mechi hiyo kwa dakika zote tisini, aliongeza: “Washambuliaji wa Simba pia wamefanya kazi nzuri na kila mmoja alikuwa bora kwa nafasi yake, ila tunapokuja kucheza uwanja wa kwao tutaongeza umakini zaidi.”
 
Simba itarudiana na Esperance Jumapili wiki hii, Februari Mosi, 2026 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
 
Simba ina wakati mgumu katika kundi D la michuano hiyo kwani katika mechi tatu, haina pointi ikiburuza mkia, huku Stade Malien ikiongoza na pointi saba, ikifuatia Esperance (5) na Petro Atletico (4).
 
Baada ya kucheza na Esperance, Simba itaifuata Petro Atletico, kisha itamalizia nyumbani dhidi ya Stade Malien.
 
Katika kikosi cha Simba, kimefanyiwa maboresho ya kusajiliwa nyota wapya dirisha hili dogo la usajili ambao ni Nickson Kibabage, Clatous Chama, Djibrilla Kassali, Libasse Gueye na Ismael Toure.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 01/29/2026