Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
WAKATI kikosi cha Yanga kikiondoka leo jijiji Dar es Salaam kuelekea Zanzibar tayari kwa mchezo wa marudiano wa
Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Pedro Goncalves, amesema anataka kuimaliza mechi hiyo kipindi cha kwanza.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Pedro amesema anataka kutumia dakika 45 za kwanza ili kupata ushindi kwani wapinzani wao watakuwa wakipambana na hali ya hewa.
“Tulipoteza kwao, lakini hatujakata tamaa ya kupata ushindi nyumbani, Jumamosi ni siku nyingine, tuna mchezo mwingine na timu hii, tunatakiwa kusahau yaliyopita na kutazama yanayokuja.
Hatutaiogopa Al Ahly kwa kuwa ni timu kubwa, siku zote ukitaka kuwa timu kubwa kama wao ni lazima uwafunge, tunajiandaa kushinda mchezo huo, haitakuwa rahisi lakini tutafanya liwezekanalo kupata pointi tatu,” alisema kocha huyo raia wa Ureno.
Amesema wanatakiwa kutumia kipindi ambacho hali ya hewa ya joto itakuwa inawasumbua hususani kipindi cha kwanza kwani kipindi cha pili wanaweza kuizoea hali hiyo na kuwasaidia.
Yanga ilipoteza mechi Ligi ya Mabingwa Afrika Ijumaa iliyopita dhidi ya wapinzani wao hao kwa kuchapwa mabao 2-0 mechi iliyopigwa uwanja wa The Borg El Arab katika mji wa Alexandria.
Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Yanga kupoteza msimu huu kwenye hatua za makundi baada ya kuanza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR ya Morocco, Novemba 22, mwaka jana na baadaye kutoka suluhu dhidi ya JS Kabylie ya Algeria.
Ikiwa kwenye Kundi B, Yanga inaendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kuvuna pointi nne katika michezo mitatu iliyocheza.
Ushindi wowote itakaoupata Jumamosi utaiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kushindwa kufanya hivyo msimu uliopita.
Msimu uliopita Yanga ilishindwa kufuzu hatua hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi A lililokuwa na timu za Al Hilal ya Sudan, MC Alger na TP Mazembe.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.