Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
NYOTA wa Simba SC, Steven Mukwala amefikisha jumla ya mabao 13 ndani ya
ligi. Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar Juni 22 alipachika bao moja.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-0 Kagera Sugar. Bao hilo alipachika dakika ya 17 akiwa ndani ya 18. Mukwala alituma pasi ya David Kameta ambaye alipokea pasi elekezi kutoka kwa kiungo mshambuliaji Jean Ahoua.
Kameta kwenye mchezo wa funga kazi Uwanja wa KMC Complex alikomba dakika 90. Alishuhudia beki mwingine anayecheza upande wake Shomari Kapombe naye akiingia kwenye mchezo huo. Kapombe alipoingia Duchu alikuwa mchezaji huru akicheza kila eneo na alikuwa akipewa maelekezo mara nyingi na Kapombe.
Mukwala anafikisha mabao 13 kwenye ligi akiwa saw ana Leonel Ateba wa Simba SC huku akiwa saw ana Clement Mzize na Prince Dube wa Yanga SC na Jonathan Sowah wa Singida Black Stars ambaye alifunga kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.
Kinara kwenye chati ya ufungaji wa mabao ndani ya ligi ni Jean Ahoua wa Simba SC ambaye amefunga jumla ya mabao 16.
Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar hakukomba dakika 90 wala hakufunga.
Mukwala alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo dhidi ya Kagera Sugar baada ya dakika 90 ikiwa ni tuzo ya mwisho kwa Simba SC kwenye ligi wakiwa kwenye mchezo wa nyumbani ndani ya msimu wa 2024/25.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.