Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
KLABU ya Yanga imejihakikishia ubingwa wa
Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2024-2025, ikiwa ni mara ya nne mfululizo, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Kariakoo Derby uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga limefungwa na Clement Mzize dakika 88 na 67 na Pacome Zouzoua, kwa mkwaju wa penalti, kufuatia kipa wa Simba, Moussa Camara, kumchezea rafu Zouzoua ndani ya eneo la hatari.
Mwamuzi wa kati kutoka Misri, Amin Mohammed Amina, hakuwa na hiyana na kuamuru mkwaju huo wa penalti.
Ushindi huo umeifanya Yanga kuondoka na pointi zote sita dhidi ya watani wao wa jadi kwa msimu huu, baada ya awali pia kushinda mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa matokeo kama hayo. Hali hiyo imezidi kuonesha ubabe wa Yanga katika mechi za hivi karibuni dhidi ya Simba.
Kwa upande wa Simba, matokeo hayo yameongeza maumivu ya msimu kwao, kwani ni mara ya tano mfululizo wanapoteza dhidi ya Yanga, jambo linaloongeza presha kwa benchi la ufundi na wachezaji wake mbele ya mashabiki wa klabu hiyo.
Ushindi huo pia unazidi kuimarisha rekodi ya Yanga ambayo imeeendelea kuwa mwiba kwa wapinzani wake katika mechi kubwa, kikosi chake kikionekana kikiwa na nidhamu ya juu ya mchezo, ubunifu wa mashambulizi na uimara wa safu ya ulinzi.
Kwa sasa, Yanga si tu kwamba ni mabingwa wa Tanzania Bara kwa mara nyingine, bali pia wameweka wazi dhamira yao ya kutawala soka la ndani na kujenga msingi madhubuti kuelekea mashindano ya kimataifa msimu ujao.
Katika mchezo huo, kikosi cha Yanga kilichoanza kiliundwa na Djigui Diarra, Israel Mwenda, Chadrack Boka, Dickson Job, Ibrahim Abdullah, Khalid Aucho, Duke Abuya, Mudathir Yahya, Prince Dube, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli.
Simba ilianzisha kikosi kilichokuwa na Moussa Camara, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Che Fondoh Malone, Chamou Karaboue, Yusuph Kagoma, Joshua Mutale, Fabrice Ngoma, Steven Mukwala, Jean Ahoua na Elie Mpanzu.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.