Steve Barker Afunguka Subira ya Ibrahim Doumbia Simba SC - “Mpeni Muda!”


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo



Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuacha kumhukumu mapema mshambuliaji wao mpya, Ibrahim Doumbia, akisisitiza kuwa nyota huyo anahitaji muda wa kutosha kuzoea mfumo wa timu na kujenga uelewano na wenzake.
 
Doumbia ni mmoja wa wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba SC katika dirisha hili la usajili kwa ajili ya kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji kuelekea msimu wa 2026/27.
 
Mbinu za Steve Barker na Michuano ya CECAFA Kagame Cup
 
Barker ameeleza kuwa michuano ya CECAFA Kagame Cup imekuwa fursa mhimu sana kwa benchi la ufundi kupima uwezo wa kikosi chao na kuwazoesha wachezaji wapya kabla ya msimu rasmi kuanza.
 
“Hatuna muda wa kutosha wa kufanya maandalizi ya kawaida ya kabla ya msimu (pre-season). Ndio maana michuano hii ya Kagame Cup inatusaidia sana kuwapa nafasi wachezaji wapya kama Doumbia kuanza kuzoeana na wenzao na kuelewa vizuri falsafa ya uchezaji ya Simba,” alisema Barker.
 
Mpeni Muda Doumbia Aonyeshe Ubora Wake
 
Kocha huyo ameongeza kuwa maamuzi ya kumsajili Doumbia hayakufanyika kwa kukurupuka, bali yalifuatia tathmini ya kina ya kiufundi. Hivyo, ana imani kubwa kuwa baada ya muda mfupi wa kuzoea mazingira, mshambuliaji huyo ataanza kuonyesha cheche zake uwanjani.
 
Kauli hii ya Barker inaashiria kuwa Doumbia ataendelea kuonekana kwenye kikosi cha kwanza katika mechi zijazo, huku benchi la ufundi likifanya kazi ya ziada kumjengea kujiamini ili awe chachu ya mabao ndani ya Simba SC.


Beti Sasa
TSh MILIONI 10 KUSHINDANIWA. Beti TSh 1,250+, Mechi 3+ Ikijumuisha Mechi ya Simba

Published: 07/31/2026