Madrid na Barcelona katika El Clasico


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 29

Real Madrid v FC Barcelona 

Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain 
Sunday, 20 March 2022
Kick-off is at 23h00  

Real Madrid watakuwa mwenyeji wa Barcelona ugani Estadio Santiago Bernabéu katika mechi ya ligi, Machi 20.
 
Real Madrid waliichapa Real Sociedad 4-1 wakiwa nyumbani katika mechi ya ligi iliyopita ya tarehe 5 Machi na watakuwa ugenini dhidi ya Real Mallorca mnamo machi 14.
 
Madrid hawajashindwa katika mechi saba za ligi zilizopita huku wakiandikisha ushindi katika mechi tano na kupata sare katika mechi mbili.


Karim-Benzema-of-Real-Madrid.jpg
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, Madrid hawajashindwa katika mechi 24 za ligi wakiwa nyumbani baada ya kuandikisha ushindi mara kumi na saba na sare saba kama wenyeji.
 
Kwengineko, Barcelona waliishinda CA Osasuna 4-0 katika mechi ya ligi iliyochezwa mnamo Machi 13.
 
Ushindi huo ulipeleka Barcelona mechi 12 za ligi bila kushindwa baada ya kuandikisha sare nne na ushindi katika mechi nane.

Barcelona hawajashindwa katika mechi 10 za ligi wakiwa ugenini huku wakiandikisha sare mara tano na ushindi mara tano wakiwa wenyeji.


xavi.jpg
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Kabla ya kucheza na Galatasaray tulipunguza kasi ya mchezo wet una nilishasema awali kuwa kasi ikipungua wapinzani wako watakukabili vilivyo,” alisema meneja wa Barcelona Xavi Hernandez baada ya ushindi dhidi ya Osasuna.
 
"Tulicheza mechi nzuri dhidi ya Osasuna. Ulikuwa mchezo mzuri tangu nimekuwa kocha wa Barcelona. Wachezaji na mashabiki wamefurahia mchezo huu na utatupa motisha zaidi.  
 
"Kati ya wapinzani wetu, ni Sevilla peke yake iliyotushinda na tulihitaji ushindi kwani ulikuwa muhimu. Tumeanza wiki yenye umuhimu vizuri sana. Tutachagua timu bora ya wachezaji kumi na moja tukizingatia mazingira yanayotukumba.”
 
Mchezo wa ligi wa mwisho baina ya Barcelona na Madrid ulikuwa mnamo Oktoba 24 2021.
 
Madrid walishinda Barcelona 2-1 ugani Camp Nou ambao ulitumika kuandaa fainali ya ligi ya klabu bingwa barani ulaya, UEFA mwaka 1989 na 1999.

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi

Mechi - 5 
Barcelona - 0
Madrid - 4
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 03/17/2022