Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
KATIKA kilele cha mafanikio ya kihistoria, Meneja wa klabu ya Simba, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa safari yao kwenye michuano ya
Kombe la Shirikisho Afrika bado haijakamilika licha ya kufuzu kwa mara ya pili kwenye fainali ya michuano hiyo.
Simba iliingia fainali baada ya ushindi wa jumla wa bao 1-0 dhidi ya Stellabocsh FC, uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kupitia bao la Jean Ahoua, huku mechi ya marudiano ikimalizika kwa sare ya 0-0 nchini Afrika Kusini.
Ahmed amesema kwamba lengo lao si tu kufuzu fainali, bali ni kuvunja historia kwa kubeba kombe hilo na kulibakiza Tanzania. Mara ya mwisho Simba kufika fainali ilikuwa mwaka 1993 miaka 32 iliyopita lakini safari hii wana kiu ya kuandika historia mpya.
“Tumefanikiwa kufikia rekodi yetu ya 1993, sasa ni muda wa kuvunja historia yetu wenyewe na kuchukua ubingwa. Tuna timu bora, tukishikamana na kupambana kwa nguvu zote, inawezekana.” Amesema.
Akitambua ubora wa wapinzani wao RS Berkane kutoka Morocco, Ahmed amesema Simba iko tayari kwa vita hiyo ya kihistoria. Mechi ya kwanza ya fainali itachezwa Morocco Mei 17, marudiano yakipangwa kuchezwa Tanzania Mei 25.
Ahmed anaiona kama fursa ya Simba kutawazwa mabingwa mbele ya mashabiki wao: “Tunajua ubora wa RS Berkane, lakini sisi ni Simba tunabeba. Mei 25 ni siku ya ubingwa nyumbani, kwa kumalizia nyumbani. Ninawaamini wachezaji wetu kama tungekuwa Ligi ya Mabingwa tungetinga hadi fainali,” amesema.
Amewataka mashabiki wa Simba kufanya kila kitu kwa asilimia mia moja ili kuhakikisha kombe linabaki nyumbani.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.