Gunners wapania kisasi dhidi ya Reds


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 9

Arsenal v Liverpool

Emirates Stadium
London, England
Sunday, 9 October 2022
Kick-off is at 18h30 

Arsenal itakuwa na mtihani mkubwa watakapoialika Liverpool ugani Emirates kwenye mechi ya ligi kuu England Jumapili Oktoba 9. 

The Gunners wanaendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali la ligi baada ya kuwashinda wapinzani wao wa jadi Tottehnam 3-1 wikendi iliyopita katika mchezo wa dabi wa 192.

Vijana wa Mikel Arteta wanaongoza ligi kwa alama moja mbele ya Manchester City baada ya mechi nane na kushinda mechi saba na kupoteza moja tangu msimu kuanza.

Gabriel Jesus
Hakimiliki ya picha: Getty Images


Arteta alisema kuwa ilikuwa siku nzuri kufuatia ushindi huo na kuwapongeza mashabiki wa nyumbani kwa kuwashabikia wachezaji kwa nguvu wakati wa mechi hiyo.

"Ilikuwa siku nzuri. Tulicheza vizuri chini ya mazingira mazuri yaliyosababishwa na mashabiki wet una hatimaye tukapata ushindi,” Arteta aliambiwa tovuti ya klabu hiyo.
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds

"Nina furaha kubwa kwa sababu kushinda mechi dhidi ya Spurs kuna maana kubwa. Kuwapa furaha mashabiki wetu kunaridhisha sana. Nahisi hizo ni hisia za kila mmoja.

"Huu ni mchezo tofauti na michezo mingine kwa sababu hisia zipo juu kwa timu zote. Unahusu kila mmoja kutoka mashabiki na wote walio na mapenzi na timu hizi.

"Siku ya mechi hii inatoa fursa kwetu wachezaji kuwapa tabasamu mashabiki zetu. Ni jukumu letu kufanya hivyo. Nahisi wachezaji walifanya vizuri kwenye jukumu hilo.”

Kwingineko, The Reds wanaonekana kutofanya vizuri baada ya kupata sare ya 3-3 dhidi ya Brighton Jumamosi iliyopita. Sare hii ilikuwa ya pili mfululizo ukizingatia sare dhidi ya Everton kabla ya mapumziko ya ligi. 

Roberto Firmino of Liverpool
Hakimiliki ya picha: Getty Images


Liverpool hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi nne zilizopita japokuwa wanajipata alama 11 nyuma ya viongozi wa ligi huku wakiwa katika nafasi ya tisa kwenye jedwali.

Klopp amekiri kuwa ukosefu wa kuwa na muendelezo wa uchezaji mzuri katika mechi unawaponza na matokeo hayawezi kuwa mazuri iwapo hawatatatua tatizo hilo.

"Tunayo kazi kubwa mbele yetu. Hilo halina mjadala. Tuanataka kupata matokeo mazuri na kuwa na alama zaidi. Tunataka kuimarisha nafasi yetu kwenye jedwali la ligi,” alisema raia huyo wa Ujerumani.

"Tunapambana kuimarisha hali yetu na hilo litatokea iwapo tutacheza vizuri. Hio ndio hali halisi.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi

Mechi - 5
Arsenal - 1
Liverpool - 4
Sare - 0

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.


Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 10/07/2022