Latest Soccer News
Habari za hivi punde za Michezo

Djokovic apania kushinda tuzo la nne mfululizo

14/01/2022 16:11:52
Mchezaji numba moja duniani wa tenisi Novak Djokovic anapania kushinda taji la Australian Open mara ya kumi ambayo itakuwa ni rekodi kwenye shindano la kwanza la Grand Slam la mwaka linazoanza januari 17.
 

Valencia na Sevilla kumenyana katika mechi kali ya La liga

14/01/2022 13:20:10
Valencia CF atakuwa mwenyeji wa Sevilla FC katika mechi ya La liga januari 19 ugani Estadio de Mestalla. 
 

Hornets kuikabili Orlando

13/01/2022 15:33:24

Charlotte Hornets watakabiliana na Orlando Magic katika mechi ya NBA ugani Spectrum Center, Charlotte katika jimbo la North Carolina. Mechi hiyo itang’oa nanga jumamosi asubui januari 15 2022 saa nane kamili majira ya afrika ya kati.

Na kutetea taji lake Waialae Country Club, Hawaii

13/01/2022 15:25:27
Kevin Na atatetea taji lake la Sony Open, Hawaii katika shindano litakalojumuisha washindi 10 wa zamani. 
 

Manchester City kuendeleza ubabe wao

13/01/2022 15:16:52
Manchester city watakuwa mwenyeji wa Chelsea katika mechi ya ligi ugani Etihad kunako januari 15 huku wakipania kuendeleza ubabe wake kwenye ligi.

Nigeria wataathari uwezo wa Sudan

13/01/2022 14:31:14
Nigeria wanatarajia kushinda mchezo wao wa pili katika mashindano ya AFCON watakapoikabili Sudan ugani Roumde Adjia katika mechi ya kundi D januari 15.