Habari za hivi punde za Soka
Habari za hivi punde za Michezo

Super Eagles kumenyana na Pharaohs

07/01/2022 16:20:31
Nigeria watapambana vikali na Misri kundi D, katika uwanja wa Roumde Adjia, Garoua kwenye mashindano ya kombe la mataifa barani afrika mnamo Jumanne 11 2022. Mechi itaanza saa kumi na mbili majira ya afrika mashariki. 

Juventus wanuia ushindi wa tatu dhidi ya Roma

07/01/2022 16:12:48
Juventus watatarajia kupata ushindi wa tatu mfululizo dhidi ya Roma watakapokutana uwanjani Stadio Olimpico januari 9 katika mechi ya ligi. 

Real Madrid wapania kurudi na ushindi

07/01/2022 16:05:24
Real Madrid watapania kurudi na ushindi baada ya kupoteza mechi yao ya pili ya msimu katika ligi watakapoialika Valencia ugani Santiago Bernabeu januari 8. 

76ers na Spurs kuchuana vikali

05/01/2022 13:26:14
Philadelphia 76ers na San Antonio Spurs watamenyana vikali katika mechi ya NBA kwenye uwanja wa Wells Fargo Philadelphia, Pennsylvania jumamosi januari 8 2022. Mechi hiyo itaanza saa nane kamili alfajiri majira ya afrika ya kati. 

Rahm apania kushinda taji la Tournament of Champions

05/01/2022 13:20:13
Mchezaji namba moja wa golfu duniani Jon Rahm anapania kushinda taji la Tournament of Champions kwa mara ya kwanza kabisa. 

Napoli wasaka ushindi muhimu Turin

04/01/2022 08:25:04
Napoli watakuwa wageni wa Juventus ugani Allianz Stadium katika mechi ya ligi jioni ya Alhamisi januari 6 2022. Mechi itang’oa nanga saa nne kasorobo, majira ya afrika ya kati.